Kushuka kwa Allaah usiku wa nusu ya Sha´baan kupitia upokezi wa Abu Muusa al-Ash´ariy


94 – Ahmad bin Muhammad bin Ziyaad al-Qattwaan ametuhadithia: al-Hasan bin ´Aliy bin Shabiyb ametuhadithia: Nimemsikia Sulaymaan bin ar-Rabiy´ al-Jiyziy akisema: Abul-Aswad ametuhadithia: Ibn Lahiy´ah ametuhadithia, kutoka kwa az-Zubayr bin Sulaym, kutoka kwa adh-Dhwahhaak bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa baba yake: Nimemsikia Abu Muusa al-Ash´ariy akisema: Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Mola wetu hushuka katika mbingu ya chini ya dunia usiku wa nusu Sha´baan ambapo akawasamehe watu wa ardhini isipokuwa mshirikina au ambaye moyoni mwake mna chuki.”[1]

[1] Ibn Abiy ´Aaswim (510). al-Albaaniy akasema:

”Hadiyth ni Swahiyh” (Dhwilaal-ul-Jannah (510))

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 173
  • Imechapishwa: 13/01/2021