Kushuka kwa Allaah usiku wa nusu ya Sha´baan kupitia upokezi wa Abu Bakr as-Swiddiyq 02

76 – Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Yuunus bin ´Abdil-A´laa ametuhadithia: ´Abdullaah bin Wahb ametuhadithia: ´Amr bin al-Haarith amenikhabarisha, kutoka kwa ´Abdul-Malik bin ´Abdil-Malik, kutoka kwa al-Musw´ab bin Abiy Dhi’b, kutoka kwa al-Qaasim bin Muhammad, kutoka kwa baba yake au ami yake, kutoka kwa babu yake, kutoka kwa Abu Bakr ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) anashuka kwenye usiku wa nusu Sha´baan katika mbingu ya chini na akamsamehe kila mtu isipokuwa kafiri au mtu ambaye moyoni mwake mna chuki.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 157
  • Imechapishwa: 02/05/2020