Kushuka kwa Allaah usiku wa nusu Sha´baan kupitia mapokezi ya Abu Bakr as-Swiddiyq

75- Abu Bakr ´Abdullaah bin Sulaymaan bin al-Ash´ath ametuhadithia: Ahmad bin Swaalih ametuhadthia, kutoka kwa ´Abdullaah bin Wahb: ´Amr bin al-Haarith amenikhabarisha, kutoka kwa ´Abdul-Malik bin ´Abdil-Malik, kutoka kwa al-Musw´ab bin Abiy Dhi’b, kutoka kwa al-Qaasim bin Muhammad, kutoka kwa baba yake au ami yake, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) anashuka kwenye usiku wa nusu Sha´baan katika mbingu ya chini na akamsamehe kila mmoja isipokuwa mtu ambaye moyoni mwake mna chuki au kumshirikisha Allaah.” [1]

[1] as-Sunnah (509) ya Ibn Abiy ´Aaswim. Shaykh al-Albaaniy amesema:

”Hadiyth ni Swahiyh lakini cheni ya wapokezi wake ni dhaifu kwa sababu ya ´Abdul-Maalik bin ´Abdil-Maalik na al-Musw´ab bin Abiy Dhi´b ambao hawajulikani… Hata hivyo nimeisahihisha Hadiyth kwa sababu imepokelewa kutoka kwa Maswahabah wengine wanane. Hadiyth imekaguliwa katika “as-Swahiyhah” (1144).”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 153-154
  • Imechapishwa: 30/04/2020
  • taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy