Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Salamah, babu yake na ´Abdul-Hamiyd bin Yaziyd

74 – Abul-Hasan ´Aliy bin Muhammad bin Ahmad al-Miswriy ametuhadithia: Maalik bin Yahyaa bin Maalik as-Suudisiy ametuhadithia: ´Aliy bin ´Aaswim ametuhadithia: ´Uthmaan al-Battwiy ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdul-Hamiyd, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake: Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Allaah (´Azza wa Jall) katika ile theluthi ya usiku anashuka katika mbingu ya chini na anakunjua mkono Wake mpaka kuingie alfajiri: “Je, kuna mwenye kuomba aniombaye nimuitikie? Je, kuna mtubiaji anayetubu nimsamehe? Je, kuna mwenye kuomba msamaha nimsamehe?”Inapoingia alfajiri hupanda.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni dhaifu kwa sababu ya kutokujulikana kwa baadhi ya wapokezi.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 151-152
  • Imechapishwa: 30/04/2020
  • taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy