Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Rifaa´ah al-Juhaniy 4

71 – ´Abdullaah bin Muhammad bin Ziyaad ametuhadithia: Muhammad bin Ghaalib ametuhadithia: Muusa bin Ismaa´iyl ametuhadithia …:

Pia Abu Sahl Ahmad bin ´Abdillaah bin Ziyaad ametuhadithia: Muhammad bin Ghaalib ametuhadithia: Muusa bin Ismaa´iyl Abu Salamah ametuhadithia: Abaan bin Yaziyd ametuhadithia: Yahyaa bin Abiy Kathiyr ametuhadithia: Hilaal bin Abiy Maymuunah amemweleza kwamba ´Atwaa’ bin Yasaar amemsimulia kuwa Rifaa´ah bin ´Araabah al-Juhaniy amemweleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kunapopita theluthi ya usiku, au nusu ya usiku, basi hushuka Allaah (´Azza wa Jall) katika mbingu ya chini na anasema mpaka kunaingia alfajiri: “Simuulizi yeyote juu ya waja Wangu zaidi yangu Mwenyewe. Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe? Ni nani mwenye kuniomba nimuitikie? Ni nani mwenye kuniomba nimpe?”

Abu Bakr an-Naysaabuury ametwambia kuhusu Hadiyth iliyosimuliwa na Hishaam, al-Awzaa´iy na ´Aliy bin al-Mubaarak kwamba inasema:

“Kunapopita nusu ya usiku, au theluthi ya usiku… “

Katika Hadiyth ya Shaddaad na Abaan imesimuliwa kwa aina ifuatayo:

“Kunapopita theluthi ya usiku, au nusu ya usiku… “

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 148-149
  • Imechapishwa: 29/04/2020