4- Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Muhammad bin Askaab ametuhadithia: Yuunus bin Muhammad na ´Affaan bin Muslim ametuhadithia: Hammaad bin Salaman ametuhadithia, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka kwa Naafiy´ bin Jubayr bin Mutw´im, kutoka kwa baba yake aliyesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola wetu (Tabaarak wa Ta´ala) kila usiku hushuka katika mbingu ya dunia na husema: mpaka alfajiri inaingia: “Hakuna mwenye kuuliza apewe? Hakuna mwenye kuomba msamaha asamehewe?”[1]

[1] Ahmad (4/81), Ibn Abiy ´Aaswim (507), ad-Daarimiy (1488) na Ibn Khuzaymah, uk. 133. Mlolongo wa wapokezi Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 93
  • Imechapishwa: 13/01/2018
  • taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy