5- Muhammad bin Nuuh ametuhadithi: Ahmad bin Muhammad bin Yahyaa bin Sa´iyd ametuhadithia: ´Affaan ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka kwa Naafiy´ bin Jubayr bin Mutw´im, kutoka kwa baba yake aliyeeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola wetu (Tabaarak wa Ta´ala) kila usiku hushuka katika mbingu ya dunia na husema: mpaka alfajiri inaingia: “Hakuna mwenye kuuliza apewe? Hakuna mwenye kuomba msamaha asamehewe?”[1]

Muhammad bin Sa´duun amesema:

“Niliandika nukuu hii ya Muhammad bin Nuuh kutoka katika hati ya mkono ya ad-Daaraqutwniy.”

[1] Ahmad (4/81), Ibn Abiy ´Aaswim (507), ad-Daarimiy (1488) na Ibn Khuzaymah, uk. 133. Mlolongo wa wapokezi Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 94
  • Imechapishwa: 13/01/2018
  • taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy