6- Muhammad bin Nuuh al-Junb Yasaabuuriy ametuhadithia: ´Aliy bin Harb al-Junb Yasaabuuriy na Ahmad bin Muhammad bin Yahyaa bin Sa´iyd ametuhadithia…

Vilevile al-Husayn bin Ismaa´iyl pia ametuhadithia: ´Aliy bin Muslim na  ´Abdul-A´laa´ bin Waaswil ametuhadithia…

al-Husayn bin Ibraahiym bin al-Husayn al-Khallaal ametuhadithia Waasitw: Ishaaq bin Wahb al-´Allaaf ametuhadithia…

Vilevile Abu Bakr an-Naysaabuuriy na wengineo wametuhadithia: ´Abbaas bin Muhammad ametuhadithia: Muhaadhir bin al-Muwarriy´ ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Abu Swaalih aliyeyataja kutoka kwa Abu Sa´iyd na Abu Hurayrah, na Abu Ishaaq na Habiyb, kutoka kwa al-Agharr, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyesema kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) huzuia mpaka kunapoenda theluthi ya mwisho ya usiku. Kisha anaterema katika mbingu ya dunia na husema mpaka alfajiri inaingia: “Hakuna mwenye kuomba maghfirah nimghufurie? Hakuna mwenye kuomba nimpe? Hakuna mwenye kutubia nimsamehe?”[1]

Wakasema:

Muhaadhir bin al-Muwarriy ametuhadithia: al-A´mash amesema:

“Naona kuwa Sufyaan ameeleza kutoka kwa Jaabir kwamba hayo yanapitika katika kila usiku.”

[1] Abu Daawuud (4733) na Ibn Khuzaymah, uk. 127. Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Khuzaymah.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 95-96
  • Imechapishwa: 16/12/2019