7- Ahmad bin Muhammad bin Mas´adah na ´Abdur-Rahmaan bin al-Hasan bin Ahmad al-Hamdaaniy wametuhadithia: Ibraahiym bin al-Hasan al-Hamdaaniy ametuhadithia: Muhammad bin Ismaa´iyl al-Ja´fariy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Maslamah bin Aslam ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin ´Abdillaah bin ´Abdir-Rahmaan bin ´Abdir-Rahmaan bin Ka´b bin Maalik, kutoka kwa Jaabir bin ´Abdillaah al-Answaariy ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Allaah hushuka kila usiku katika mbingu ya dunia kwenye theluthi ya usiku na kusema: “Hakuna mja katika waja Wangu anayeniomba nimuitikie? Au ambaye ameidhulumu nafsi yake aniombae nimghufurie? Au fakiri ili nimruzuku? Au aliyedhulumiwa aniombae nusura nimnusuru? Au mwenye huzini aniombae ili nimsahilishie?” Hiyo ndio inakuwa sehemu Yake mpaka kunaposwaliwa Fajr. Kisha Mola wetu (´Azza wa Jall) anakuwa juu ya mbingu, juu ya Kursiy Yake.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 96-97
  • Imechapishwa: 16/12/2019