Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa ´Amr bin ´Abasah

66 – Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Ahmad bin Mansuur ametuhadithia: Yaziyd bin Haaruun, Yahyaa bin Abiy Bukayr na ´Abdus-Swamad bin an-Nu´maan ametuhadithia: Jariyr bin ´Uthmaan ametuhadithia: Sulaymaan bin ´Aamir ametuhadithia, kutoka kwa ´Aamir bin ´Abasah aliyesema:

“Nilimwendea Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nikasema: “Ee Mtume wa Allaah, Allaah anifanye kuwa fidia kwako! Nifunze kitu ambacho sikijui na ambacho kitaninufaisha na hakitonidhuru? Ni wakati gani bora wa mtu kuwa mchaji zaidi?” Akasema: “Ee ´Amr bin ´Abasah! Hakika umeuliza jambo ambalo hakuna yeyote aliyeniuliza kabla yako. Hakika Mola hushuka katikati ya usiku na akamsamehe kila mmoja isipokuwa mshirikina tu. Na swalah ni yenye kushuhudiwa mpaka kuchomoze jua.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 142
  • Imechapishwa: 28/04/2020