Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa ´Amr bin ´Abasah 02

67 – ´Aliy bin ´Abdillaah bin Mubashshir ametuhadithia: Ahmad bin Sinaan ametuhadithia: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: Jariyr bin ´Uthmaan ametuhadithia: Sulaymaan bin ´Aamir ametuhadithia, kutoka kwa ´Aamir bin ´Abasah aliyesema:

“Nilimwendea Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipokuwa ´Ukaadhw nikasema: “Ni nani ambaye amekufuata katika jambo hili?” Akasema: “Muungwana na mtumwa.” Hapakuwa mwengine zaidi ya Abu Bakr na Bilaal. Kisha akasema: “Ondoka zako mpaka pale Allaah atapomthibitisha Mtume Wake.” Baada ya hapo akaja kwa mara nyingine na kusema: “Ee Mtume wa Allaah, Allaah anifanye kuwa fidia kwako! Nifunze kitu ambacho sikijui na ambacho kitaninufaisha na hakitonidhuru? Ni wakati gani bora wa mtu kuwa mchaji zaidi?” Akasema: “Ee ´Amr bin ´Abasah! Hakika umeuliza jambo ambalo hakuna yeyote aliyeniuliza kabla yako. Hakika Mola hushuka sehemu ya mwisho ya usiku na akamsamehe kila mmoja isipokuwa mshirikina na mkandamizaji. Na swalah ni yenye kuandikwa na ni yenye kushuhudiwa mpaka kuchomoze jua. Huchomoza kati ya mapembe mawili ya shaytwaan na hapo ndipo makafiri huswali. Kipindi hicho usiswali mpaka jua lichomoze. Linapochomoza jua basi swalah hushuhudiwa mpaka pale linapoanza tena kuzama. Linazama kati ya mapembe mawili ya shaytwaan. Kipindi hicho usiswali mpaka jua lizame.”[1]

[1] Ahmad (4/385).  Mlolongo wa wapokezi ni Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 143-144
  • Imechapishwa: 28/04/2020