Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa ´Aliy bin Abiy Twaalib 3

3- ´Aliy bin ´Abdillaah al-Fadhwl ametuhadithia Misri: Muhammad bin Wakiy´ ametuhadithia: Muhammad bin Ismaa´iyl bin Ibraahiym bin Muusa bin Ja´far bin Muhammad bin ´Aliy bin al-Husayn bin ´Aliy bin Abiy Twaalib ametuhadithia: Ami wa Abul-Husayn bin Muusa amenihadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu wa Ja´far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Aliy bin al-Husayn, kutoka kwa ´Aliy ambaye amesema: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Allaah (´Azza wa Jall) hushuka katika mbingu ya dunia kila usiku wa ijumaa, kuanzia mwanzo wake mpaka mwisho wake, na katika nyusiku zengine katika theluthi ya mwisho ya usiku. Halafu anamwamrisha Malaika kusema: “Hakuna mwenye kuomba msamaha nimsamehe? Hakuna mwenye kuomba maghfirah nimghufurie? Ee wewe mwenye kutaka kheri, jitokeze mbele. Ee wewe mwenye kutaka shari, koma.”[1]

[1] al-´Ayniy amesema:

”Katika mlolongo wa wapokezi kuna wapokezi wasiojulikana.” (´Umdat-ul-Qaariy (7/287))

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 92
  • Imechapishwa: 05/12/2017