Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa ´Aliy bin Abiy Twaalib 2

2- Abu Sahl Ahmad bin Muhammad bin ´Abdillaah bin Ziyaad ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Ishaaq ametuhadithia: ´Aliy bin ´Abdillaah ametuhadithia: Ya´quub bin Ibraahiym bin Sa´d ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia, kutoka kwa Muhammad bin Ishaaq: Ahmad bin Muhammad bin Abiyr-Rijaal ametuhadithia: Sulaymaan bin Yuusuf al-Harraaniy ametuhadithia: Sa´iyd bin Baziy ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq: ´Abdur-Rahmaan bin Yasar amenihadithia, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin Abiy Raafiy´, kutoka kwa ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh): Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Lau nisingelichelea kuwatia uzito Ummah wangu basi ningeliwaamrisha kutumia Siwaak wakati wa kila swalah na kuchelewesha ´Ishaa mpaka theluthi ya kwanza ya usiku. Pindi kunapopita theluthi ya usiku, basi Allaah (´Azza wa Jall) hushuka katika mbingu ya chini ya dunia na hubaki huko mpaka alfajiri inaingia na anasema mwenye kusema: “Hakuna mwenye kuuliza apewe maombi yake? Hakuna mwenye kuomba ajibiwe? Hakuna mgonjwa aponywe?”

Muhammad bin Sa´duun amesema:

“Niliandika Hadiyth hii kutoka kwenye hati ya mkono ya ad-Daaraqutwniy.”

Wakasema:

Muhaadhir bin al-Muwarriy ametuhadithia: al-A´mash amesema:

“Naonelea Sufyaan ameieleza kutoka kwa Jaabir ya kwamba hayo yanapitika kila usiku.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 91-92
  • Imechapishwa: 05/12/2017