Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa ´Aliy bin Abiy Twaalib 1


1- Abu Bakr (bin) ´Abdillaah bin Muhammad bin Ziyaad an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Ahmad bin Mansuur ametuhadithia: Ya´quub bin Ibraahiym bin Sa´d ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Ishaaq: Ami yangu amenihadithia, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin Abiy Raafiy´, mawla wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Lau nisingelichelea kuwatia uzito Ummah wangu basi ningeliwaamrisha kutumia Siwaak wakati wa kila swalah na kuchelewesha ´Ishaa mpaka theluthi ya kwanza ya usiku. Pindi kunapopita theluthi ya usiku, basi Allaah (´Azza wa Jall) hushuka katika mbingu ya chini ya dunia na hubaki huko mpaka alfajiri inaingia na anasema: “Hakuna mwenye kuuliza apewe? Hakuna mwenye kuomba ajibiwe? Hakuna mgonjwa aponywe? Hakuna mtenda dhambi mwenye kuomba msamaha asamehewe?”[1]

[1] al-Haythamiy amesema:

”Imepokelewa na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Awsatw”. Katika mlolongo wa wapokezi kuna Ishaaq ambaye ni mwaminifu na mudallis. Hapa anasema wazi ni nani aliyemueleza.  Hata hivyo mlolongo wa wapokezi ni mzuri.” (Majma´-uz-Zawaa-id (1/221))

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 89-90
  • Imechapishwa: 05/12/2017