73 – Abul-Hasan ´Aliy bin Muhammad bin Ahmad al-Miswriy ametuhadithia: Rawh bin al-Faraj Abuz-Zanaabiy´ ametuhadithia: Yahyaa bin Bukayr ametuhadithia: al-Layth bin Sa´d ametuhadithia: Ziyaad bin Muhammad amenihadithia, kutoka kwa Muhammad bin Ka´b al-Quradhwiy, kutoka kwa Fadhwaalah bin ´Abdillaah al-Answaariy, kutoka kwa Abud-Dardaa’, kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) hushuka katika ile saa ya theluthi ya usiku inayobaki. Basi Anafungua uandishi katika ile saa ya kwanza ambayo hakuna mwengine aliyeiona zaidi Yake; Allaah anakifuta akitakacho na anathibitisha akitakacho. Katika ile saa ya pili anashuka katika Pepo yenye mabustani; ndio nyumba Yake ambayo hakuna jicho lolote limekwishayaon wala haijampitikia yeyote kwenye moyo wake. Pia ndio makazi Yake ambayo hakuna hakuna mwanadamu yeyote atakaa Naye isipokuwa watu aina tatu: Mitume, wakweli na mashahidi. Kisha anasema: “Twuubaa kwa yule mwenye kuingia ndani yako!” Katika ile saa ya tatu Yeye, akiwa pamoja na Roho na Malaika Zake, wanashuka katika mbingu ya chini ambapo inaanza kutikisika. Kisha anaiambia: “Ninaapa kwa utukufu Wangu! Inuka!” Kisha anawaangalia waja Wake na anasema mpaka wakati wa swalah ya Fajr: “Je, kuna mwenye kuomba msamaha nimsamehe? Hakuna mwenye kuniuliza nimpe? Je, hakuna mwenye kuomba aniombaye nimuitikie?” Kwa ajili hiyo Allaah (Ta´ala) anasema:

إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا

“Qur-aan ya alfajiri, kwani hakika Qur-aan ya alfajiri ni yenye kushuhudiwa.”[1]

Anaishuhudia Allaah na Malaika Zake; Malaika wa usiku na mchana.”[2]

[1] 17:78

[2] Jaamy´-ul-Bayaan (15/139) kupitia kwa al-Layth bin Sa´d.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 153-154
  • Imechapishwa: 30/04/2020