Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa ´Uqbah bin ´Aamir

65 – Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Muhammad bin ´Abdil-Malik al-Waasitwiy ametuhadithia: Abul-Husayn Haaruun al-Khazzaaz ametuhadithia kwa njia ya kutusomea kitabu chake: ´Aliy bin al-Mubaarak ametuhadithia: Yahyaa bin Abiy Kathiyr ametuhadithia: Hilaal bin Abiy Maymuunah amenihadithia kwamba ´Atwaa’ bin Yasaar amemweleza kuwa ´Uqbah bin ´Aamir amemsimulia:

“Tulikuwa pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi aliposema: “Kunapopita theluthi ya usiku (au alisema “Kunapopita nusu ya usiku”) basi hushuka Allaah (´Azza wa Jall) katika mbingu ya chini na anasema mpaka kunaingia alfajiri: “Simuulizi yeyote juu ya waja Wangu zaidi yangu Mwenyewe. Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe? Ni nani mwenye kuniomba nimuitikie? Ni nani mwenye kuniomba maghfirah nimghufurie?

Abu Ja´far amesema:

“Namna hii ndivo alivotusomea Haaruun kutoka katika kitabu chake na akamtaja ´Uqbah bin ´Aamir.”

Watu wengi, akiwemo Hishaam ad-Dastawaa’iy, ´Abdur-Rahmaan al-Awzaa´iy na Abaan al-´Attwaar, ameipokea kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa Hilaal bin Abiy Maymuunah, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Yasaar, kutoka kwa Rifaa´ah bin ´Araabah al-Juhaniy (Radhiya Allaahu ´anh). Ndicho kilichohifadhiwa.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 140-141
  • Imechapishwa: 28/04/2020