52 – Abu ´Abdillaah al-Husayn bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Yuusuf bin Muusa ametuhadithia: Jariyr ametuhadithia, kutoka kwa Mansuur, kutoka  kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa Abu Muslim al-Agharr, kutoka kwa Abu Sa´iyd na Abu Hurayrah waliosimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) anawapa muhula mpaka kunapopita theluthi ya kwanza ya usiku ndipo hushuka katika mbingu ya chini ya dunia na anasema mpaka alfajiri inaingia: “Je, kuna mwenye kutubia? Je, kuna mwenye kuomba msamaha? Je, kuna mwenye kuomba?”[1]

[1] Muslim (172).

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 231
  • Imechapishwa: 10/03/2020