Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Abu Sa´iyd na Abu Hurayrah 13

64 – Muhammad bin al-´Abbaas bin Muhammad ametuhadithia: Muhammad bin Abiy Bakr al-Waasitwiy ametuhadithia: Muhammad bin ´Abdillaah al-Maqdisiy ametuhadithia: Maalik bin Sa´iyd ametuhadithia: al-A´mash ametuhadithia, kutoka kwa Abu Swaalih, kutoka kwa Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd pia kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa al-Agharr, kutoka kwa Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd, pia kutoka kwa Habiyb bin Abiy Thaabit, kutoka kwa al-Agharr, kutoka kwa Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) hutoa muhula mpaka kunapopita nusu ya usiku ndipo anashuka katika mbingu ya dunia ya chini na anasema mpaka inachomoza alfajiri: “Je, kuna mwenye kuomba msamaha nimsamehe? Je, kuna mwenye kuomba ajibiwe? Je, kuna mwenye kuomba msamaha nimsamehe?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 138-139
  • Imechapishwa: 28/04/2020