Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Abu Sa´iyd na Abu Hurayrah 11

62 – al-Husayn bin Ismaa´iyl ametuhadithia: ´Abdul-´Alaa bin Waaswil na ´Aliy bin Muslim ametuhadithia …:

Pia Muhammad bin al-Jund Yasaabuuriy ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad bin Yahyaa bin Sa´iyd ametuhadithia …:

Pia Abu Bakr an-Naysaabuuriy na wengineo wametuhadithia: al-´Abbaas bin Muhammad bin Haatim ametuhadithia: Muhaadhwir bin al-Muawarri´ ametuhadithia: al-A´mash ametuhadithia, kutoka kwa Abu Swaalih aliyetaja kutoka kwa Abu Sa´iyd au Abu Hurayrah…:

Pia Abu Ishaaq naa Habiyb bin Abiy Thaabit wamepokea kutoka kwa al-Agharr, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) hutoa muhula mpaka kunapopita nusu ya kwanza ya usiku kisha anashuka katika mbingu ya dunia ya chini na anasema: “Je, kuna mwenye kuomba msamaha nimsamehe? Je, kuna mwenye kuuliza nimpe? Je, kuna mwenye kuomba msamaha nimsamehe?”[1]

[1] Ibn Abiy ´Aaswim (1/500-501). Cheni ya wapokezi ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 137-138
  • Imechapishwa: 28/04/2020