Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Abu Sa´iyd na Abu Hurayrah 08

59 – Abul-Aswad ´Ubaydullaah bin Muusa bin Ishaaq al-Answaariy na Ahmad bin Kaamil wametuhadithia: Muhammad bin Sa´d al-´Awfiy ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia: Sulaymaan bin Qarm ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa Abu Muslim al-Agharr, kutoka kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy na Abu Hurayrah ambao wamemshuhudilia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mimi nashuhudia kwamba wamesema: Tumemsikia akisema:

“Mola wenu (´Azza wa Jall) hutoa muhula mpaka kunapopita theluthi ya usiku ya kwanza ndipo hushuka katika mbingu ya dunia ya chini na anasema: “Je, kuna mtenda dhambi anayetubu? Je, kuna mwenye kuuliza? Je, kuna mwenye kuomba msamaha? Je, kuna mwenye kuomba?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 135
  • Imechapishwa: 26/04/2020