Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Abu Sa´iyd na Abu Hurayrah 07

58 – Ahmad bin Muhammad bin Ziyaad ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Ishaaq ametuhadithia: Musaddad ametuhadithia: Abu ´Awaanah ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq al-Hamadaaniy, kutoka kwa Abu Muslim al-Agharr aliyesema:

“Namshuhudilia Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd al-Khudriy kwamba wawili hao wamemshuhudilia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema: “Allaah (´Azza wa Jall) anatoa muhula mpaka kunapopita (au kubaki) theluthi ya usiku ndipo hushuka na husema: “Je, kuna mwenye kuomba aitikiwe? Je, kuna mwenye kuomba apewe? Je, kuna mwenye kuomba msamaha kutokamana na dhambi?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 134-135
  • Imechapishwa: 26/04/2020