Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Abu Sa´iyd na Abu Hurayrah 05

56- al-Husayn bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Ahmad bin Mansuur ametuhadithia: ´Abdur-Razzaaq ametuhadithia: Ma´mar ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa Abu Muslim al-Agharr, kutoka kwa Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd al-Khudriy ambao wameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) anatoa muhula mpaka kunapopita theluthi ya mwisho ya usiku ndipo hushuka katika mbingu hii ya chini ya dunia na anasema mpaka kwapambazuka: “Je, kuna mwenye kuomba msamaha asamehewe? Je, kuna mwenye kuomba maghfiyrah? Je, kuna mwenye kuomba? Je, kuna mwenye kuuliza?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 133
  • Imechapishwa: 26/04/2020