Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Abu Sa´iyd na Abu Hurayrah 04

55 – Abu Bakr bin ´Abdillaah bin Muhammad bin Ziyaad ametuhadithia: ´Abbaas bin Muhammad bin Haatim bin Shabaabah ametuhadithia: Yuunus bin Abiy Ishaaq ametuhadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Muslim al-Agharr aliyesema:

“Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd al-Khudriy wameshuhudia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na mimi nashuhudia kwamba wamesema,  kuwa Allaah (´Azza wa Jall) anawapa muhula mpaka kunapopita theluthi ya kwanza ya usiku ndipo hushuka katika mbingu ya chini ya dunia. Kisha anaamrisha milango ya mbingu inafunguliwa kish anasema mpaka alfajiri inaingia: “Je, kuna mwenye kuomba nimpe? Je, kuna mwenye kuomba nimuitikie? Je, kuna mwenye kuomba msamaha nimsamehe? Je, kuna mwenye kutaka msaada nimsaidie? Je, kuna aliye na dhiki nimwondolee dhiki yake? Anafanya hivo katika kila usiku kisha anapanda tena juu.”

Yuunus bin Abiy Ishaaq ameongeza ziada nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 133
  • Imechapishwa: 12/03/2020