Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Abu Sa´iyd na Abu Hurayrah 03

Muslim bin Ibraahiym ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa al-Agharr aliyesema:

“Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd al-Khudriy wameshuhudia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na mimi nashuhudia kwamba wamesema,  kuwa Mola (´Azza wa Jall) hushuka katika mbingu ya chini ya dunia kila usiku katika theluthi ya usiku na anasema: “Kisha anaita mwenye kuita: “Je, hakuna mwenye kuomba msamaha asamehewe? Je, hakuna mwenye kuuliza apewe? Je, hakuna mwenye kuomba aitikiwe?”[1]

[1] Muslim (172).

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 132-133
  • Imechapishwa: 12/03/2020