Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Abu Sa´iyd na Abu Hurayrah 02

53 – Muhammad bin Nuuh an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad bin Yahyaa bin Sa´iyd ametuhadithia: Husayn bin ´Aliy ametuhadithia, kutoka kwa Fudhwayl…

Pia al-Husayn bin Ismaa´iyl ametuhadithia: ´Abdullaah bin Muhammad bin Shaakir ametuhadithia: Husayn (yaani Ibn ´Aliy al-Ju´fiy) ametuhadithia: Fudhwayl bin ´Iyaadhw ametuhadithia, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa Abu Muslim al-Agharr aliyeeleza:

“Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd al-Khudriy wameshuhudia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na mimi nashuhudia kwamba wamesema,  kuwa Allaah (´Azza wa Jall) anawapa muhula mpaka kunapopita theluthi ya kwanza ya usiku ndipo hushuka katika mbingu ya chini ya dunia na anasema mpaka alfajiri inaingia: “Je, kuna mwenye kuomba msamaha? Je, kuna mwenye kuuliza? Je, kuna mwenye kuomba?”[1]

[1] ash-Shariy´ah, uk. 310, ya al-Aajurriy.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 132
  • Imechapishwa: 12/03/2020