Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Abu Hurayrah


13 – 317 Abu Muhammad Yahyaa bin Muhammad bin Sa´iyd alisomewa mimi huku nasikiliza: Yahyaa bin Sulaymaan al-Khuzaa´iy ametuhadithia: Sulaymaan bin Bilaal ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Ahmad bin ´Alqamah, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) anashuka kila usiku katika mbingu ya dunia kwenye nusu ya usiku au theluthi ya mwisho na anasema mpaka alfajiri inaingia au anaondoka mwenye kuswali kutoka katika swalah ya asubuhi: “Ni nani aniombaye nimuitikie? Ni nani aniombae nimpe? Ni nani aniombae maghfirah nimghufurie?”[1]

[1] Ahmad (2/504) na Ibn Khuzaymah (1/302) aliyeisahihisha.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 102
  • Imechapishwa: 16/01/2018