Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Abu Hurayrah 5


17- Ibn Saa´id alisomewa na mimi huku nasikiliza: al-Hasan bin Muhammad az-Za´faraaniy na Muhammad bin ´Abdil-Malik ad-Daqiyqiy wamekuhadithieni: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: Muhammad bin ´Amr ametuhadithia, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) anashuka kila usiku katika mbingu ya dunia kwenye nusu ya usiku au theluthi ya mwisho na anasema mpaka alfajiri inaingia: “Ni nani aniombaye nimuitikie? Ni nani aniombae nimpe? Ni nani aniombae maghfirah nimghufurie?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 104
  • Imechapishwa: 17/01/2018