50 – Muhammad bin Sahl bin al-Fadhwl na Muhammad bin ´Abdillaah bin al-Husayn al-´Allaaf wametuhadithia: Humayd bin ar-Rabiy´ ametuhadithia: Khaalid bin Makhlad ametuhadithia: Muhammad bin Ja´far bin Abiy Kathiyr ametuhadithia: Suhayl amenihadithia kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam) amesema:

“al-Jabbaar anashuka kila usiku kunapopita theluthi ya usiku au nusu yake na anasema mpaka alfajiri inaingia: “Je, kuna mwenye kuomba nimpe? Je, kuna aliyefanya dhambi aombae msamaha nimsamehe?[1]

[1] Ahmad (2/504) na Ibn Khuzaymah (1/302) aliyeisahihisha.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 129
  • Imechapishwa: 10/03/2020