47 – Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Ahmad bin Mansuur ametuhadithia: Ya´quub bin Ibraahiym bin Sa´iyd ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia, kutoka kwa Muhammad bin Ishaaq: Sa´iyd bin Abiy Sa´iyd al-Maqbariy amenihadithia kutoka kwa ´Atwaa’, mtumwa wa Umm Swubayyah, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyemweleza kwamba alimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Lau nisingelichelea kuwatia uzito Ummah wangu basi ningeliwaamrisha kutumia Siwaak wakati wa kila swalah na kuchelewesha ´Ishaa mpaka theluthi ya kwanza ya usiku. Pindi kunapopita theluthi ya usiku, basi Allaah (´Azza wa Jall) hushuka katika mbingu ya chini ya dunia na hubaki huko mpaka alfajiri inaingia na anasema: “Hakuna mwenye kuuliza apewe? Hakuna mwenye kuomba ajibiwe? Hakuna mgonjwa aponywe? Hakuna mtenda dhambi mwenye kuomba msamaha asamehewe?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 127-128
  • Imechapishwa: 09/03/2020