46 – Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Muhammad bin Yahyaa ametuhadithia: Ya´quub bin Ibraahiym bin Sa´iyd ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq aliyesema: Sa´iyd bin Abiy Sa´iyd al-Maqbariy amenihadithia, kutoka kwa ´Atwaa’, mtumwa wa Umm Sabiyyah aliyeachwa huru, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyemweleza kwamba alimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Lau kama mimi sikuchukia kuwatia uzito Ummah wangu basi ningeliwaamrisha kutumia Siwaak wakati wa kila swalah na wacheleweshe swalah ya ´Ishaa mpaka theluthi ya usiku. Pindi kunapopita theluthi ya usiku, basi Allaah hushuka katika mbingu ya chini ya dunia na anasema: “Hakuna mwenye kuomba du´aa ajibiwe? Hakuna mwenye kuomba apewe? Hakuna mgonjwa aponywe? Hakuna mtenda dhambi mwenye kuomba msamaha asamehewe?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 126
  • Imechapishwa: 28/01/2020