43 – ´Abdus-Swamad bin ´Aliy ametuhadithia: al-Fadhwl bin al-´Abbaas at-Twustariy ametuhadithia: Yahyaa bin Ghaylaan ametuhadithia: ´Abdullaah bin Baziy´ ametuhadithia: Rawh bin al-Qaasim ametuhadithia, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin ´Umar, kutoka kwa Sa´iyd al-Maqbariy, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyeeleza kuwa Mtume (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Lau nisingeliona uzito juu ya Ummah wangu basi ningeliwaamrisha kutumia Siwaak pamoja na wudhuu´ na ningechelewesha swalah ya ´Ishaa mpaka theluthi ya usiku au nusu ya usiku. Hakika Allaah (´Azza wa Jall) wakati huo hushuka katika mbingu ya dunia na kusema: “Je, kuna mwenye kuomba nimuitikie? Je, kuna mwenye kuomba nimpe maombi yake? Je, kuna mwenye kuomba msamaha nimsamehe?”

Baqiyyah ameipokea kutoka kwa ´Ubaydullaah, kutoka kwa al-Maqbariy, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Hurayrah.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 125
  • Imechapishwa: 27/01/2020