15- Abu Muhammad bin Saa´ida alisomewa na mimi huku nasikiliza: Ibraahiym bin Sallaam al-Makkiy amekuhadithieni: ´Abdul-´Aziyz bin Muhammad ad-Daraawardiy ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin ´Amr, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyeeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) anashuka kila usiku katika mbingu ya dunia kwenye nusu ya usiku au theluthi ya mwisho na anasema mpaka alfajiri inaingia: “Ni nani aniombaye nimuitikie? Ni nani aniombae nimpe? Ni nani aniombae maghfirah nimghufurie?”[1]

[1] al-Albaaniy amesema:

“Mlolongo wa wapokezi ni mzuri na Swahiyh.” (Dhwilaal-ul-Jannah (496))

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 104
  • Imechapishwa: 16/01/2018