41- al-Qaadhwiy Husayn bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Abus-Swaa-ib Saalim bin Junaadah ametuhadithia: ´Abdullaah bin Numayr ametuhadithia, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin ´Umar, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Sa´iyd, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Lau nisingeliona uzito juu ya Ummah wangu basi ningeliwaamrisha kutumia Siwaak pamoja na wudhuu´ na ningechelewesha swalah ya ´Ishaa mpaka theluthi ya usiku au nusu ya usiku. Hakika Allaah (´Azza wa Jall) wakati huo hushuka katika mbingu ya dunia na kusema: “Je, kuna mwenye kuomba nimuitikie? Je, kuna mwenye kuomba nimpe maombi yake? Je, kuna mwenye kuomba msamaha nimsamehe?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 124
  • Imechapishwa: 27/01/2020