39- al-Husayn bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Muhammad bin Yaziyd (ndugu yake Karkhuuyah) ametuhadithia…

Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Sa´daan bin Naswr ametuhadithia: Ishaaq al-Azraq ametuhadithia: ´Ubaydullaah ametuhadithia, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Sa´iyd al-Muqriy, kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Lau nisingeliona uzito juu ya Ummah wangu basi ningeliwaamrisha kutumia Siwaak pamoja na kila wudhuu´ na ningeliwaamrisha kuchelewesha swalah ya ´Ishaa mpaka nusu ya usiku, au theluthi ya usiku. Hakika Allaah (´Azza wa Jall) hukaribia katika mbingu ya dunia na kusema mpaka alfajiri inaingia: “Je, kuna mwenye kuomba nimuitikie? Je, kuna mwenye kuomba nimpe?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 123
  • Imechapishwa: 21/01/2020