38– Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Ziyaad an-Naysaabuuriy ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Bishr bin al-Hakam ametuhadithia…

Ibraahiym bin Hammaad pia ametuhadithia: Abu Muusa amenihadithia…

Ya´quub bin Ibraahiym an-Najjaad pia ametuhadithia: ´Umar bin Shabbah ametuhadithia…

Pia Abu ´Ubayd bin al-Muhaayil, ´Aliy bin ´Abdillaah bin Mubashshir na Ya´quub bin Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab ad-Duuriy wametuhadithia: Hafsw bin ´Umar ametuhadithia: Yahyaa bin Sa´iyd al-Qattwaan ametuhadithia: ´Ubaydullaah ametuhadithia: Sa´iyd amenihadithia, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kunapopita theluthi ya usiku au nusu ya usiku hushuka Allaah (´Azza wa Jall) katika mbingu ya dunia na kusema: ”Je, kuna mwenye kuomba nimpe? Je, kuna mwenye kuomba msamaha nimsamehe? Je, kuna mwenye kutubia nimsamehe? Kuna mwenye kuomba nimuitikie?”

Hili ni tamko la an-Naysaabuuriy. Waliobaki wamepokea kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Lau nisingeliona uzito juu ya Ummah wangu basi ningeliwaamrisha kutumia Siwaak pamoja na kila wudhuu´ na ningechelewesha swalah ya ´Ishaa mpaka theluthi, au nusu ya usiku. Kunapopita theluthi ya usiku au nusu ya usiku basi hushuka Allaah (´Azza wa Jall) katika mbingu ya dunia na kusema mpaka alfajiri inaingia: ”Je, kuna mwenye kuomba msamaha nimsamehe? Je, kuna mwenye kuomba nimuitikie? Je, kuna mwenye kuomba msamaha nimsamehe?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 122-123
  • Imechapishwa: 21/01/2020