37- Abul-Qaasim Naswr bin Babzuuyah ash-Shiyraaziy ametuhadithia: Ishaaq bin Ibraahiym Shaadhaan ametuhadithia: Abu Daawuud ametuhadithia: Ibraahiym bin Sa´d ametuhadithia, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Abu Salamah bin ´Abdir-Rahmaan na al-A´raj, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyemweleza kwamba alimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Mola wetu (Ta´ala) hushuka pindi kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku na husema: “Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe?  Ni nani mwenye kuniomba nimpe? Ni nani mwenye kiniomba nimuitikie?”

Abu Ishaaq as-Sabiy´iy na Habiyb bin Abiy Thaabit vilevile wameipokea Hadiyth hii kutoka kwa al-Agharr, kutoka kwa Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd al-Khudriy. Nitaziandika pamoja na Hadiyth za Abu Sa´iyd al-Khudriy baada ya kuzimaliza Hadiyth za Abu Hurayrah.

Sa´iyd bin Abiy Sa´iyd al-Muqriy pia ameipokea Hadiyth hii. Wametofautiana juu yake; ´Ubaydullaah bin ´Umar  amesema kuhusu Sa´iyd: Kutoka kwa Sa´iyd al-Muqriy, kutoka kwa Abu Hurayrah. Muhammad bin Ishaaq amepokea kutoka kwa Sa´iyd al-Muqriy, kutoka kwa ´Atwaa´, mtumwa wa Umm Swabiyyah aliyeachwa huru, kutoka kwa Abu Hurayrah.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 120-122
  • Imechapishwa: 19/01/2020