Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa Abu Hurayrah 24


36- Abu Muhammad bin Swaa´id ametukhabarisha: Muhammad bin ´Aliy bin Hasan bin Shaqiyq al-Marwaziy na Abu Subh Ahmad bin Mansuur bin Raashid al-Marwaziy wametuhadithia: an-Nadhwr bin Shumayl ametuhadithia: Swaalih ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Yaziyd al-Laythiy, kutoka kwa Abu ´Abdillaah al-Agharr, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Hakika Allaah (´Azza wa Jall) hushuka kila usiku pindi kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku katika mbingu ya dunia na husema mpaka alfajiri inaingia: “Ni nani mwenye kuniomba nimuitikie? Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe?”

Abu Daawuud at-Twayaalisiy pia ameipokea kutoka kwa Ibraahiym bin Sa´d, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Abu Salamah na al-Agharr.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 119-120
  • Imechapishwa: 19/01/2020