35- Abu Muhammad bin Swaa´id ametukhabarisha: Yuusuf ametuhadithia: Swafwaan bin Swaalih ametuhadithia: al-Waliyd bin Muslim ametuhadithia: Ibn Sam´aan ametuhadithia: az-Zuhriy amenikhabarisha, kutoka kwa al-Agharr, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu ushukaji wa al-Jabbaar (Jalla wa ´Azz) katika theluthi ya mwisho ya usiku. Kwa ajili hiyo Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakifadhilisha kuswali sehemu ya mwisho ya usiku kuliko mwanzoni mwake.

Swaalih bin Abiyl-Akhdhwar pia ameipokea kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Yaziyd al-Laythiy, kutoka kwa Abu ´Abdillaah al-Agharr, kutoka kwa Abu Hurayrah kufuatiliwa katika hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 118-119
  • Imechapishwa: 19/01/2020