33- Haafidhw Abu Twaalib Ahmad bin Naswr ametuhadithia: Ahmad bin Ziyaad al-Hadhdhaa’ na Abu Usaamah al-Halabiy ametuhadithia…

Abu Muhammad bin Swaa´id na Abu ´Abdillaah Muhammad bin Ismaa´iyl al-Faarisiy ametuhadithia: Abu Usaamah ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiy Usaamah al-Halabiy ametuhadithia: Hajjaaj bin Abiy Maniy´ ar-Rasaafiy ametuhadithia: Babu yangu ´Abdullaah bin Abiy Ziyaad amenihadithia, kutoka kwa az-Zuhriy: Abu Salamah bin ´Abdir-Rahmaan bin ´Awf az-Zuhriy na Abu ´Abdillaah al-Agharr, Swahibah wa Abu Hurayrah, ameeleza kwamba Abu Hurayrah amemweleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola wetu (´Azza wa Jall) hushuka kila usiku pindi kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku katika mbingu ya dunia na husema mpaka alfajiri inaingia: “Ni nani mwenye kuniomba nimuitikie? Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe? Ni nani mwenye kiniomba nimpe?”

Mu´aawiyah bin Yahyaa as-Sadafiy pia ameipokea kutoka kwa az-Zuhriy.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 117
  • Imechapishwa: 16/01/2020