32 – Abu Muhammad bin Swaa´id na huku nikisikiliza: Muhammad bin Khaalid bin ´Aliy al-Kalaa-iy amekuhadithieni Himsw: Bishr bin Shu´ayb bin Abiy Hamzah ametuhadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa az-Zuhriy…

Pia alisomewa Ibn Swa´iyd: Muhammad bin ´Abdil-Malik bin Zanjuuyah na Muhammad bin ´Awf bin Sufyaan wamekuhadithieni…

Abu Bakr an-Naysaabuuriy pia ametuhadithia: Ahmad bin Yuusuf as-Sulamiy na Ibraahiym bin Haani’ wametuhadithia: Abul-Yamaan ametuhadithia: Shu´ayb ametukhabarisha, kutoka kwa az-Zuhriy: Abu Salamah bin ´Abdir-Rahmaan na al-Agharr Abu ´Abdillaah, Swahibah wa Abu Hurayrah, amenihadithia kwamba Abu Hurayrah amemukhabarisha kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) hushuka kila usiku pindi kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku katika mbingu ya dunia na husema: “Ni nani mwenye kuniomba nimuitikie? Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe? Ni nani mwenye kiniomba nimpe?”

´Ubaydullaah bin Abiy Ziyaad ar-Rasaafiy pia ameipokea kupitia kwa az-Zuhriy.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 116
  • Imechapishwa: 16/01/2020