30- Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Wahb bin Yaziyd bin Khaalid ametuhadithia: ´Abdullaah bin Wahb ametuhadithia: Yuunus na Maalik wamenikhabarsha…

Au Bakr an-Naysaabuuriy pia ametuhadithia: Ahmad bin ´Abdir-Rahmaan bin Wahb ametuhadithia: Ami yangu ametuhadithia: Yuunus amenihadithia, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Abu Salamah na al-Agharr ambaye ameeleza kwamba wamemsikia Abu Hurayrah akisema: Mtume wa Allaah (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola wetu (´Azza wa Jall) hushuka pindi kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku katika mbingu ya dunia na husema: “Ni nani mwenye kuniomba nimpe? Ni nani mwenye kuniomba nimuitiie? Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe?”[1]

al-Layth bin Sa´d vilevile ameipokea kupitia kwa Yuunus.

[1] al-Bukhaariy (1145) na Muslim (521).

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 114
  • Imechapishwa: 15/01/2020