29- Abu Muhammad bin Swaa´id alisomewa na mimi huku nikisikiliza: Muhammad bin Sahl amenihadithia, kutoka kwa ´Askar al-Bukhaariy, Muhammad bin ´Abdil-Malik bin Zanjuuyah, Zuhayr bin Muhammad, al-Hasan bin Abiyr-Rabiy´ na al-Hasan bin Mansuur (ambaye tamko ni lake)…

Abu Bakr an-Naysaabuuriy pia ametuhadithia: Muhammad bin Yahyaa na Ahmad bin Mansuur ametuhadithia: ´Abdur-Razzaaq bin Hammaam ametuhadithia: Ma´mar ametuhadithia, kutoka kwa az-Zuhriy: Abu Salamah bin ´Abdir-Rahmaan na al-Agharr Abu ´Abdillaah, Swahibah wa Abu Hurayrah, wamenikhabarisha kwamba Abu Hurayrah amewakhabarisha kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Mola wetu (´Azza wa Jall) hushuka kila usiku pindi kunapobaki theluthi ya usiku katika mbingu ya dunia na husema: “Ni nani mwenye kuniomba nimuitikie? Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe? Ni nani mwenye kuniomba nimpe?”

Yuunus bin Yaziyd al-Ayliy vilevile ameipokea kutoka kwa az-Zuhriy.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 113
  • Imechapishwa: 15/01/2020