26- Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Yuunus bin ´Abdil-A´laa´ ametuhadithia: ´Abdullaah bin Wahb ametuhadithia: Maalik amenikhabarisha, kutoka kwa az-Zuhriy.

Abu Rawq Ahmad bin Muhammad bin Bakr pia ametuhadithia Baswrah: Muhammad bin Muhammad bin Khallaad ametuhadithia: Ma´iyn bin ´Iysaa ametuhadithia: Maalik ametuhadithia…

Abu Muhammad bin Swaa´id pia ametuhadithia, kutoka kwa Muusa bin Abiy Khuzaymah: Yahyaa bin Yahyaa ametuhadithia: Nilimsomea Maalik…

Ahmad bin Muhammad bin Ja´far al-Jawziy pia ametuhadithia: Ibraahiym bin Ishaaq as-Sarraaj ametuhadithia…

´Ubaydullaah bin ´Abdis-Swamad bin al-Muhtadiy bil-Laah ametuhadithia: ´Aliy bin al-Husayn bin Mihraan an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Yahyaa bin Yahyaa ametuhadithia: Nilimsomea Maalik…

Abu Muhammad bin Swaa´id vilevile ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdil-Malik bin Zanjuuyah na Ahmad bin Mansuur wametuhadithia: al-Qa´naabiy ametuhadithia, kutoka kwa Maalik.

´Uthmaan bin Ahmad ad-Daqqaaq na Ahmad bin Muhammad bin Ziyaad pia wametuhadithia: Ismaa´iyl bin Ishaaq ametuhadithia: ´Abdullaah bin Maslamah ametuhadithia, kutoka kwa Maalik.

Muhammad bin ´Aliy bin Ismaa´iyl al-Ayliy ametuhadithia: ´Ubaydullaah bin Muhammad bin Ibraahiym as-Swan´aaniy ametuhadithia: Ibn Maslamah Abu Qudaamah ametuhadithia: Yahyaa bin Maalik bin Anas ametuhadithia: Baba yangu amenikhabarisha…

al-Hasan bin Rushayq pia ametuhadithia Misri: Ahmad bin Muhammad bin ´Abdil-´Aziyz ametuhadithia: Yahyaa bin Bukayr ametuhadithia: Maalik ametuhadithia…

al-Hasan bin ´Aliy bin Daawuud at-Tarraaz pia ametuhadithia Misri: Ahmad bin Yahyaa bin Jariyr ametuhadithia: al-Haarith bin Miskiyn ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin al-Qaasim ametuhadithia: Maalik ametuhadithia…

Baada ya hapo wakasema:

“… kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Abu ´Abdillaah al-Agharr, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu Hurayrah.

Ibn-ut-Twabbaa´, al-Qa´nabiy na Yahyaa bin Maalik bin Anas amesema, kutoka kwa Maalik, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Abu Salamah, kutoka kwa Abu ´Abdillaah al-Agharr, kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola wetu (´Azza wa Jall) hushuka kila usiku katika mbingu ya chini ya dunia kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku na anasema: “Ni nani mwenye kuniomba nimuitikie? Ni nani mwenye kunitaka kitu nimpe? Ni nani aniombae maghfirah nimghufurie?”

Hili ni tamko la Ibn Wahb. Waliobaki wameipokea kwa “ni nani” bila “na”.

Vilevile ameipokea Bishr bin ´Umar, kutoka kwa ´Abdullaah bin Yuusuf at-Tinniysiy, kutoka kwa Maalik, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa al-Agharr peke yake, kutoka kwa Abu Hurayrah.

Pia ameipokea ´Abdul-Malik bin Ziyaad an-Nusaybiy, kutoka kwa Maalik, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Abu Salamah peke yake, kutoka kwa Abu Hurayrah.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 108-110
  • Imechapishwa: 01/01/2020