Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa ´Abdullaah bin Mas´uud

8- ´Abdullaah bin Muhammad bin Ziyaad al-Faqiyh ametuhadithia: Abu Umayyah at-Twartuusiy amenihadithia: Mu´aawiyah bin ´Amr ametuhadithia: Zaa-idah ametuhadithia: Ibraahiym al-Hajariy ametuhadithia, kutoka kwa Abul-Ahwnas, kutoka kwa ´Abdullaah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) huifungua milango ya mbingu kisha anashuka katika mbingu ya dunia, halafu anaikunjua mikono Yake na kusema mpaka alfajiri inaingia: “Hakuna mja mwenye kuniomba nimpe?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 98-99
  • Imechapishwa: 15/01/2018