Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa ´Abdullaah bin Mas´uud 5

12- Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Yaziyd bin Sinaan ametuhadithia Misri: Abu Bakr al-Hanafiy ametuhadithia: ´Abdul-Hamiyd bin Ja´far ametuhadithia: al-Maqbariy amenihadithia, kutoka kwa ´Awn bin ´Abdillaah bin ´Utbah, kutoka kwa Ibn Mas´uud aliyesema:

“Siku moja wakati tulipokuwa tumeketi msikitini pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja mwanamume kutok katika Banuu Sulaym akiitwa ´Amr bin ´Utbah. Alikuwa amemfuata (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Makkah na hakumuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa mpaka alipofika al-Madiynah. Akaja na kusema: “Ee Mtume wa Allaah! Nifunze kitu unachojua ambacho mimi sikijui  na ambacho kitaninufaisha, na wala usirefushe. Ni swalah ipi ya mchana au usiku ambayo ni salama zaidi?” Mwishoni akasema: “Ni swalah ya sunnah ambayo ni bora zaidi?” Akasema: “Wakati kunapoenda theluthi ya usiku (au alisema “nusu ya usiku”). Katika wakati huo hushuka Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall) katika mbingu ya dunia na kusema: “Hakuna mtenda dhambi aniombae msamaha nimghufurie? Hakuna mwombaji ambaye analililia Nimpe maombi yake? Au hakuna mwenye huzuni nimsahilishie?” Mpaka alfajiri inapoingia Mwingi wa huruma hupanda, Aliye mtukufu, Aliye juu kabisa (´Azza wa Jall).”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 100-101
  • Imechapishwa: 15/01/2018