Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa ´Abdullaah bin Mas´uud 4

11- Abul-Hasan ´Aliy bin Muhammad bin Ahmad al-Muqriy ametuhadithia: Maalik bin Yahyaa Abu Ghassaan ametuhadithia: ´Aliy bin ´Aaswim ametuhadithia: Ibraahiym bin Muslim al-Hajariy ametuhadithia, kutoka kwa Abul-Ahwas, kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uud ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Inapofika theluthi ya usiku wa mwisho uliyobaki Allaah (´Azza wa Jall) hushuka katika mbingu ya dunia, anaikunjua mikono Yake akisema: “Hakuna mwombaji aniombae nimuitikie? Hakuna mwenye kuomba maghfirah nimghufurie? Hakuna mwenye kutubia nimsamehe?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 100
  • Imechapishwa: 15/01/2018