Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa ´Abdullaah bin Mas´uud 2


9- Muhammad bin Nuuh al-Jund Yasaabuuriy ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad bin Yahyaa bin Sa´iyd ametuhadithia: Husayn Abu ´Aliy ametuhadithia, kutoka kwa Zaa-idah, kutoka kwa Ibraahiym al-Hajariy, kutoka kwa Abul-Ahwas, kutoka kwa ´Abdullaah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) huifungua milango ya mbingu katika ile theluthi ya usiku wa mwisho uliyobaki. Kisha Anashuka katika mbingu ya dunia ambapo anaikunjua mikono Yake na kusema mpaka alfajiri inaingia: “Hakuna mja mwenye kuniomba nimpe?”[1]

[1] Ahmad Shaakir amesema:

“Mlolongo wa wapokezi ni dhaifu kwa sababu ya udhaifu wa al-Hajariy. Hata hivyo maana yake imepokelewa kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.” (Musnad-ul-Imaam Ahmad” (1/447))

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 99
  • Imechapishwa: 15/01/2018