Kushirikiana katika biashara na mtu mwenye mali ya haramu

Swali: Kuna rafiki yangu mmoja ameniomba tushirikiane katika biashara moja hivi. Lakini mali yake ni ya haramu. Je, inajuzu kwangu kushirikiana naye kwa kuwa kuna mwanafunzi mmoja amejuzisha ushirikiano huu kwa hoja ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya biashara na mayahudi na mali yao ilikuwa ni ya haramu.

Jibu: Huu ni uongo. Mali yote ya mayahudi haikuwa ya haramu, kulikuwa na mali ya haramu na ya halali. Mtu akiwa na mali iliyochanganyika – halali na haramu – hakuna neno kushirikiana naye na kula chakula chake kwa kuzingatia ile ya halali. Kwa kuwa huwezi kuyakinisha kuwa ni ile ya haramu. Asli ni uhalali [Ibaah]. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anakula chakula cha mayahudi na akanunua kutoka kwao. Kwa kuwa sio kila walichonacho ni haramu, wana halali sehemu kubwa na wana haramu pia. Ama ikijulikana ya kwamba mali ya mtu huyu yote ni haramu, haijuzu kwako kula kutoka kwenye mali hiyo, kukubali zawadi kutoka kwake wala kununua kutoka kwake kitu. Kwa kuwa ni ya haramu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-10-15.mp3
  • Imechapishwa: 10/11/2014