Kushika kiganja cha mkono wakati wa kukaa kati ya sijda mbili

Swali: Ni yepi maoni sahihi kuhusu kushika kitanga cha kuume wakati wa kukaa kati ya sijda mbili?

Jibu: Hakuna kushika kitanga katika kikao kati ya sijda mbili. Kushika kitanga inakuwa wakati wa kusimama. Hapa ndipo anatakiwa kushika kiganja cha kuume kwa kiganja cha kushoto na baadaye aweke juu ya kifua na aweke ncha za vidole kwa nyuma kidogo au juu yake kwenye maunganishio.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (06) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/433/433.mp3
  • Imechapishwa: 08/12/2018