Swali: Baadhi ya waislamu wanasherehekea sikukuu ya kuzaliwa – yaani krismasi kama wanavyoiita, tunaomba nasaha?

Jibu: Haijuzu kwa muislamu mwanamme na mwanamke kushirikiana na manaswara au mayahudi au makundi mengine katika sikukuu zao. Ni wajibu kuacha hilo kwa kuwa [Mtume amesema]:

“Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni miongoni mwao.”

Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katukataza kushirikiana nao, kuchukua tabia zao. Ni juu ya muumini mwanamme na mwanamke kujiepusha na hilo wala wasihudhurie katika sikukuu zao kwa chochote. Kwa kuwa sikukuu zao zinakhalifu Shari´ah ya Allaah isitoshe ni maadui wa Allaah. Kwa hiyo haijuzu kushiriki humo wala kusaidizana nao wala kuwasaidia kwa lolote; si kwa [kunywa] hata chai, kahawa na kadhalika. Pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَتَعَاوَنُواْ عَلَى الْبرِّ وَالتَّقْوَى وَلاَ تَعَاوَنُواْ عَلَى الإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

”Saidianeni katika wema na uchaji Allaah wala msisaidiane katika dhambi na uadui.” (05:02)

Kushirikiana na makafiri katika sikukuu zao ni aina ya kusaidiana katika dhambi na uadui. Ni wajibu kwa waislamu wote wanamme na wanamke kuacha hilo. Wala mtu asidanganyike na wayafanyayo watu; bali ni wajibu aangalie alifanyalo – Uislamu na yale iliyokuja nayo na atekeleza amri za Allaah na Mtume Wake wala asidanganyike na mambo ya watu. Hakika watu wengi hawajali na Shari´ah ya Allaah, kama alivyosema Allaah (´Azza wa Jall) katika kitabu Chake kitukufu:

وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللّهِ

“Ukiwatii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya Allaah.” (06:116)

وَمَا أَكْثَرُ النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ

“Na wengi wa watu si wenye kuamini hata ukijitahidi vipi.” (12:103)

Ni wajibu kutekeleza Shari´ah, haijuzu kuichukulia sahali. Muislamu hufanya vitendo na kauli zake na za watu kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikiwa yataafikiana nayo (Qur-aan na Sunnah) basi yatakubaliwa hata watu wakiyaacha. Na wakiyakhalifu au wakayachukia watu, yatarudishwa [hayatokubaliwa] hata watu wakiyafanya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://youtu.be/O7jikWCbou0
  • Imechapishwa: 05/10/2020